OZIL AIPA MTIHANI ARSENAL

OZIL AIPA MTIHANI ARSENAL

427
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kawapa masharti, straika Mesut Ozil, amesema kuwa atakubali kusaini mkataba mpya na Arsenal endapo kocha wake, Arsene Wenger, atamwonesha nia ya kuendelea kuinoa klabu hiyo.

Kauli ya Mjerumani huyo imekuja baada ya Oktoba mwaka jana mtandao wa Goal .com kuripoti kuwa Ozil anajisikia mwenye furaha Arsenal, lakini alichokuwa akikitaka ni kuona suala la kocha huyo likipatiwa ufumbuzi wa haraka kabla hajajitia kitanzi kingine tena  cha kuitumikia Gunners huku mkataba wa Wenger ukimalizika miezi sita baadaye.

Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajia kumalizika majira ya joto yajayo na kama ilivyo kwa mwenzake, Alexis Sanchez, bado hawajakubali kuongeza mwingine ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Emirates, lakini wameshauambia uongozi wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa Jiji la London nia yao ya kubaki.

“Najisikia furaha kubwa kuwa hapa  Arsenal na nimeliweka wazi hilo ili klabu ifahamu kuwa nipo tayari kusaini mkataba mpya,” Ozil aliliambia jarida la Kicker.

“Mashabiki wengi wananitaka nibaki na sasa hilo litakuwa jukumu la klabu,” aliongeza nyota huyo.

Alikwenda mbali zaidi akisema kuwa pia klabu inafahamu yupo katika timu hiyo kwa sababu ya Arsene Wenger, kutokana na kwamba ndiye aliyemsajili na hivyo ni mmoja kati ya watu anaowaamini.

Alisema kuwa pia klabu vilevile inatakiwa kufahamu kuwa anataka kuwekwa wazi ni kitu gani ambacho kocha anatakiwa kukifanya katika siku za mbeleni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU