WACHEZAJI GABON, ZIMBABWE WAWEKA NGUMU

WACHEZAJI GABON, ZIMBABWE WAWEKA NGUMU

584
0
KUSHIRIKI

HARARE, Zimbabwe


WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya  Guinea Bissau na wenzao kutoka  Zimbabwe, wameingia katika mvutano na mashirikisho ya soka ya nchi zao kuhusu fedha zao zikiwa ni siku chache kabla ya kwenda nchini Gabon kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika Afcon 2017.

Shirika la habari la Ureno, Lusa, liliripoti jana kuwa mvutano huo ulitokea juzi na kuwalazimu wachezaji wa timu ya Taifa ya Guinea Bissau kwenda kumfuata rais wa nchi hiyo, Jose Mario Vaz, zikiwa ni jitihada zao kulipatia ufumbuzi suala hilo, baada ya fedha zao za bonasi  walizoahidiwa kama watafuzu kutolipwa.

Shirika hilo liliripoti kuwa wakati nchini Guinea Bissau hali ikiwa hivyo pia nchini Zimbabwe, mambo yalikuwa ni hivyo hivyo baada ya wachezaji kumwekea ngumu Kaimu Rais  Emmerson Mnangagwa, kwa kutokwenda kuhudhuria chakula cha usiku alichowaandalia wakishinikiza kupewa mgawo zaidi wakati wa mashindano hayo.

Lusa lilieleza kuwa wachezaji wanataka kulipwa dola 5000 kwa kila mechi lakini wakaahidiwa nusu yake.

Hata hivyo, hafla hiyo iliendelea kama kawaida bila wachezaji na makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba, mgawo utakwenda pande zote mbili kati ya wachezaji na chama cha soka.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU