DOGO JANJA ATAHADHARISHWA NA ‘PANYA ROAD’

DOGO JANJA ATAHADHARISHWA NA ‘PANYA ROAD’

940
0
KUSHIRIKI

HABARI ZOTE NA ZAITUNI KIBWANA


SIKU chache baada ya msanii wa hip hop kutoka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja, kubadilisha mwonekano wake kwa kuweka meno ya dhahabu, msanii huyo ametahadharishwa na vibaka ambao kwa sasa wamepewa jina  la panya road.

Tahadhari hiyo imetolewa wiki hii na mashabiki wake mara baada ya msanii huyo kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimwonyesha amebadili mwonekano huo.

Katika picha alizoweka Dogo Janja ziliambatana na ujumbe: “Acha nifanye utoto nikikua nitaacha’, zimewafanya mashabiki wake kutoa ushauri mbalimbali.

Moja ya ushauri aliopewa msanii huyo ni kutopita njia zisizoeleweka na kusababisha ‘panya road’ kumvamia na kumwibia meno hayo yaliyotajwa kuwa na thamani kubwa.

Joseph Suma aliandika kwenye ukurasa huo akisema: “Kuwa makini na mitaa utakayokatiza, maana huo mdomo sasa hivi umekuwa dili si unajua ukata umetukumba vijana.”

Licha ya Suma kumtaka kuwa makini, wapo mashabiki wengine waliomponda na kumshangaa msanii huyo kwa kitendo chake cha kuiga wenzake.

Pretty Chalres aliandika: “Yaani kitu akifanya Diamond basi lazima watu waige, huu ni ulimbukeni na hayo meno wala hayajakupendeza ungetafuta kiki kwa mengine,” aliandika. Licha ya maneno yote hayo, Dogo Janja alionekana kutokujali chochote na kuendelea kuweka picha zilizokuwa zikimwonyesha mabadiliko yake ya mdomo aliyofanya kwa sasa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU