JB MPIANA “TAJIRI, MASIKINI WOTE WANA HAKI YA KUPENDWA”

JB MPIANA “TAJIRI, MASIKINI WOTE WANA HAKI YA KUPENDWA”

462
0
KUSHIRIKI

NA NOAH YONGOLO


KONA ya Bolingo bado imepiga kambi katika Jiji la Kinshasa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikiangazia shughuli mbali mbali zinazofanywa na wanamuziki wa nchi hiyo.

Na leo tupo na mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Wenge BCBG, JB Mpiana, ambaye tungo zake nyingi zimewahi kutikisa ikiwamo ya Grace A Toi Germain.

Wimbo huu unaopatikana katika albamu iliyotoka mwaka 2000.

Wimbo huu unaelezea mambo  mengi, nami bila hiyana nakuletea tafsiri ya wimbo huu kwa lugha ya Kiswahili mstari kwa mstari ili upate kuelewa kile alichokimaanisha.

Au sommet Du Mont Blanc Je resalue November – Kileleni mwa Mont Blanc, pokea salamu zangu Novemba.

Amour eloko oyo esalema mpo na banso – Upendo ni kitu kilichoumbwa kwa ajili ya wote.

Eclaquer nga porte na zolo mawa na nga – Leo hii pendo lanifungia mlango usoni masikini mie.

Natikali isolee na Couloir ya D’ception – Najikuta mpweke niliyejaa majonzi, simanzi na masikitiko.

Bolingo eboyi kosekisa nga – Penzi limekataa kunichekesha.

Mawa efandeli nga na matama – Huzuni yajichora mashavuni mwangu.

Efungoli Robinet ya pinzoli – Imefungua bomba la machozi.

Soki ezalaki mayi ya Regideso – Kama machozi yangu yangekuwa maji ya bomba ya Regideso (Shirika la Maji DRC).

Mbele baye kolongola Compteur – Wangekuja kuyakata kwa jinsi yanavyotiririka.

Bolingo mpo nini yo okomi moselu na maboko ma nga lokola ngolo? – Penzi kwanini unateleza mikononi mwangu kama samaki?

Germain Souries Moi – Germain nioneshe tabasamu lako. Je T’en Supplie – Tafadhali.

Ba scenes ya ba Amourex nakoma komona lokola bilili ya Television– Kwangu mimi  kuwaona wawili wapendanao ni jambo ambalo silijui tena, huwa natazama kama picha kwenye runinga.

Germain Souries moi Je T’en supplie – Germain nioneshe tabasamu lako tafadhali.

Koyenga yenga lokola Kipekapeka oyo azangaka fololo – Niwapo mtaani nahaha kama kipepeo aliyekosa ua.

En me promenant nalokotaki  la photo D’un jeune tres sympa – Kutokana na mihangaiko hiyo, nimebahatika kuokota picha ya kijana maridadi.

J’Avais bien voulu que djo ango asekisa nga – Ningependa kijana aliye katika picha anioneshe tabasamu lake anichekeshe.

Foto ezalaka soured pe muette – Kumbe picha huwa haisemi, wala haisikii!

Ordinateur ya Nzambe par la Priere epesaki nga identite na ye nyoso – Baada ya kuingia kwenye maombi, nikaenda kwenye kompyuta ili nipate kujua vitambulisho vyake.

Germain Germando Rue De L’Amour ( Rue De L’Amour ) Jina lake Germain Germando, anakaa kwenye mtaa wa wapendanao.

Tu vis dans Oasis qui S ‘Appelle affection – Anaishi kwenye Oasis inaitwa upendo.

C’est Pour quoi Je T’aime ( Je Taime ) Germain Germando – Ni kwa maana hiyo nakupenda Germain Germando;

Germando T’es La Musique De mon affection – Wewe ni wimbo niupendao.

De nature aux couleurs d’un Martin pecheur Germando en – Mwenye aina na rangi ya Kingfisher Germando.

Grace A Toi Germando loboko na nga  edivorcer na litama – Kutokana na wewe Germando, kilio changu kimeshawafanya waondoe mkono wangu shavuni.

Riche ou Pauvre tout le Monde a Droit A L’amour – Tajiri kama alivyo masikini, wote wana haki ya kupendwa.

Helin kombo na nga oyebi Adjola Suba motema humm – Jina langu walijua Adjola Suba, moyo humm.

Kombo na nga oyebi Jacky Lomata ya Germando – Jina langu walijua Jacky Lomata.

Nzambe sala likamwisi,Nzambe eh sala likamwisi ooh – Mungu tenda maajabu, Mungu fanya maajabu Ooh.

Ya nga Amida akoma a zero metre na nga – Naomba mpenzi wangu Amida  awe karibu sana name.

Daida, Soraya, Junior Fari (Anawataja wanawe Daida, Soraya na Junior Fari)

Grace A Toi Germando Loboko na nga  edivorcer na litama – Kutokana na wewe Germando, kilio changu kimeisha, wafanya niondoe mkono wangu shavuni.

Mwana ya moto ata omelisi ye libele na butu – Mtoto kama si wako, hata ukimpa ziwa anyonye usiku na akapata usingizi.

Na tongo tongo akolamuka akotuna wapi baboti ba ye – Asubuhi mapema atakapoamka ataanza kulia na kuuliza wazazi wake wako wapi.

Bila shaka umemuelewa Mpiana kile alichokisimulia katika wimbo huu, kazi kwako kuutafuta na kuusikiliza ukiwa umetulia na gazeti lako hili la BINGWA.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

JIFUNZE LINGALA 10.1.2017

KARUBINI kwa mara nyingine katika  darasa letu la Lingala, naamini nyote mu wazima wa afya.

Nawasihi mchukue madaftari pamoja na kalamu zenu ili tuanze kubukua kupitia gazeti hili adhimu la Bingwa.

Kabla hatujaanza naomba niwakumbushe kitu kimoja, unapojifunza jambo lolote lazima ulifanyie mazoezi mara kwa mara  ili uweze kulimudu sawa sawa.

Mfano mdogo ni kwa mchezaji wa  soka, kama hufanyi mazoezi na kufuata maelekezo ya kocha huwezi kufanikiwa!

Maana yangu ni kwamba haya ninayokufundisha ni lazima uyafanyie mazoezi kwa vitendo ili uweze kuelewa haraka nilichokufundisha.

Tuendelee sasa na pale tulipoishia wiki iliyopita, tuanze na neno Kondima (kukubali) – Nani a kondima kozala moumbu ya Satana? – Nani atakubali kuwa mtumwa wa shetani?

Koteka (kuuza) – Nakei na zando koteka madeso – Naenda sokoni kuuza maharage.

Koloba (kusema) – Nazangi maloba ya koloba – Nimekosa maneno ya kusema.

Koboma (kuua) – Olingi koboma nga mpo na nini? – Unataka kuniua kwa sababu gani?

Komema (kuchukua) – Yaka komema ngai – Njoo unichukue.

Kotumba (kuunguza) – Mwasi na ngai oza kotumba bilei – Mke wangu unaunguza chakula.

Kolala (kulala) – Tika kolala moninga na nga, lamuka okende koluka mosala – Acha kulala rafiki yangu, amka uende kutafuta kazi.

Kolakisa (kuonesha) – Nga nabungi, nani a kolakisa ngai nzela? – Nimepotea,                      nani atanionesha njia?

Kofungola (kufungua) – Soki Nzambe azali kofungola, nani akokoka kokanga ? – Kama Mungu anafungua, nani anaweza kufunga?

Kofuta (kulipa) – Kisi ya nyongo eza kofuta – Dawa ya deni ni kulipa.

Kokata (kukata) – Tika kokata boye – Acha kukata hivyo. Kokweya (kuanguka) – Kokende mbangu te, o kokweya pamba – Usiende mbio, utaanguka bure.

Kolanda (kufuata) – Kolanda ngai te,okoya kobunga – Usinifuate, utakuja kupotea.

Kokonda (kukonda) Mikolo oyo obandi kokonda, ozo lia bileyi te? – Siku hizi umeanza kukonda, hauli chakula?

Kokoka (kuweza) – Nani a kokoka kobalola butu ekoma moyi? – Nani anaweza kuubadili usiku kuwa mchana?

Wanafunzi wangu kwa leo tuishie hapa, panapo majaaliwa tukutane tena wiki ijayo, nawatakia siku njema.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU