MANYIKA JR AMUUMBUA VIBAYA OMOG

MANYIKA JR AMUUMBUA VIBAYA OMOG

1874
0
KUSHIRIKI

NA MAREGES NYAMAKA


KIWANGO cha juu kilichoonyeshwa na kipa kinda wa Simba katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea mjini Unguja, ni kama kimemuumbua kocha wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara ambayo kwa sasa ipo kwenye mapumziko mafupi kupisha michuano ya Mapinduzi, Manyika hakuwa chaguo la Omog badala yake kocha huyo alikuwa akimpa nafasi kipa raia wa Ivory Coast, Vincent Angban, ambaye mkataba wake  ulisitishwa wakati wa usajili wa dirisha dogo.

Baada ya Angban kuondoshwa, Simba ilimsajili kipa raia wa Ghana, Daniel Agyei, ili kuziba nafasi ya Mivory Coast huyo hatua iliyopelekea Manyika kuendelea kusugua benchi.

Lakini hatua ya Omog kumpa nafasi Manyika kwenye michuano hiyo ni kama kimempa somo kwamba, alikuwa akifanya makosa kutomwamini kwani ameonyesha kiwango maridadi katika mechi zote alizosimama langoni.

Kabla ya mchezo wa leo unaotarajiwa kuzikutanisha Yanga na Simba, kinda huyo ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Peter Manyika, amewadakia Wekundu hao mechi mbili ambazo ni dhidi ya URA ya Uganda na Jang’ombe Boys Unguja.

Katika mechi zote mbili, mbali ya Simba kuibuka na ushindi, kipa huyo hakuruhusu bao hata moja huku akiisaidia timu yake kuilaza URA bao 1-0 kisha kuibanjua Jang’ombe Boys mabao 3-0.

Kwa upande wa Agyei, alisimama kwenye mechi dhidi ya timu za Taifa Jang’ambe na KVZ mchezo uliomalizika Simba kushinda mabao 2-1.

Ubora huo wa Manyika huenda ukamshawishi Omog kuendelea kumtumia hata kikosi chake kitakaporejea kwenye Ligi Kuu Bara.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU