MKUDE: MECHI DHIDI YA YANGA ITAKUWA NI YA KUFUTA  MACHUNGU

MKUDE: MECHI DHIDI YA YANGA ITAKUWA NI YA KUFUTA  MACHUNGU

953
0
KUSHIRIKI

NA JESSCA NANGAWE


NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema mchezo wao dhidi ya Yanga  hautakuwa rahisi licha ya wapinzani wao hao kufungwa mabao 4-0 na Azam FC Jumamosi iliyopita.

Simba na Yanga zitashuka dimbani leo kuumana katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja.

Mkude ameliambia BINGWA kuwa anaamini kila upande utaingia uwanjani kwa tahadhari ya kuepuka kupoteza hali itakayofanya kuwa mchezo mgumu.

Alisema kitendo cha Yanga kufungwa mabao manne na Azam kitawafanya waingie kwa nguvu kwa lengo la kupata ushindi ili kupoza machungu yao, lakini azma yao haitafanikiwa kwakuwa hata wao wanatamani kulipa kisasi baada ya kupoteza mechi zote mbili msimu uliopita.

“Haijawahi kutokea tukacheza na wapinzani wetu mchezo ukawa rahisi, mechi kama hii ni ngumu zaidi kwetu kwa sababu wenzetu wanaingia uwanjani kwanza wakiwa na machungu ya kufungwa idadi kubwa ya mabao, pili wanataka kujenga heshima yao ya kutokubali kufungwa na wapinzani wao,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU