ONYANGO ATINGA KAMBINI UGANDA CRANES

ONYANGO ATINGA KAMBINI UGANDA CRANES

568
0
KUSHIRIKI

DUBAI, Falme za Kiarabu


MLINDA mlango wa timu ya Taifa ya Uganda The Cranes, Denis Onyango, ametua katika kambi ya kikosi cha timu hiyo kilichopo mjini Dubai tayari kuongeza nguvu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika Afcon 2017.

Taarifa zinaeleza kuwa staa huyo wa timu ya Mamelodi Sundowns, aliwasili kambini hapo mapema juzi na jioni yake alitarajiwa kuanza mazoezi na wenzake.

Akizungumza na mtandao wa supersport.com, Onyango alielezea furaha yake ya kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kutwa kufunga safari kwenda nchini Gabon kwa ajili ya fainali hizo ambazo zitaanza siku moja baada ya wao kuwasili.

“Najivunia kuungana na wenzangu. Kilichobaki sasa ni kuelekeza nguvu zangu Afcon kwa sababu ni mashindano makubwa na hivyo inanibidi niwe katika ubora wangu. Kwa kufanikiwa kuwa mchezaji bora Afrika, ninatakiwa nioneshe haikuwa ni kama ajali,” alisema nyota huyo.

The Cranes itazianza fainali hizo Januari 17 mwaka huu kwa kukutana na Ghana mtanange utakaopigwa kwenye Uwanja wa Stade de Port Gentil, kabla ya Janauari 21 kutoana na Misri kwenye  dimba hilo hilo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU