SEMENYA AOA MWANAMKE MWENZIWE

SEMENYA AOA MWANAMKE MWENZIWE

1409
0
KUSHIRIKI

JOHANNESBURG, Afrika Kusini


MWANARIADHA aliyewahi kutikisa vichwa vya habari ulimwenguni kote kutokana na utata wa jinsia yake, Caster Semenya, ameendeleza maajabu baada ya hivi karibuni kuoa.

Semenya ni mwanariadha wa kike ambaye aliwahi kushutumiwa kuwa ni jinsia ya kiume hasa baada ya kuonekana kuwa na kasi kubwa katika mchezo wa riadha ambapo alishinda mbio za mita 800.

Baada ya uchunguzi wa kina wa madaktari bingwa, iligundulika kuwa licha ya jinsia na muonekano wake wa kiume, Semenya ni mwanamke.

Mwanadada huyo alifunga ndoa na mwanadada mwenzake aitwaye Violet Raseboya na imeelezwa kuwa uhusiano wao ni wa muda mrefu.

Mwanariadha huyo ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu aliangusha bonge la ‘party’ katika sherehe ya harusi ambayo pia iliambatana na siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 26.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki, ndugu na watu mashuhuri nchini Afrika Kusini.

Imelezewa kuwa mahari aliyolipa Semenya kwa msichana mwenzake huyo ni pauni 1,500 (3,958,010).

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU