UWOYA NA SIRI YA ‘KITUMBO’ 2017

UWOYA NA SIRI YA ‘KITUMBO’ 2017

1865
0
KUSHIRIKI

MASHABIKI wa supastaa wa filamu za kibongo, Irene Uwoya, mwishoni mwa wiki hii walimkalia kooni msanii huyu na kutaka ukweli wa tumbo lake kama ni mjamzito au la.

Mashabiki hao walianza gumzo hilo mara tu baada ya msanii huyo kuweka picha ikimwonyesha akiwa ‘supermarket’, huku nguo aliyoivaa ikiwa inamuonyesha kama ana ujauzito mkubwa tu.

Picha hiyo iliwaibua wale wote wanaomuunga mkono huku wengi wakimpa hongera kwa hatua ya kuanza mwaka mpya akiwa anatarajia kupata mtoto wa pili.

Lady Kapungu aliandika: “Hicho ni kitumbo cha mimba eheee, hivi wenzangu mmeona tumbo kama nilivyoona mimi au macho yangu yananidanganya?

Grace Baraka aliandika: “Itakuwa tumbo linamuuma bosi wangu, Mungu amponye au tumpeleke gym akalipunguze hakuna namna nyingine la kupunguza.

Ujumbe wote huo uliokuwa ukitumwa na mashabiki ulimfanya Uwoya kuibuka na kuandika ujumbe mfupi wenye mafumbo kuwa: “Usiamini kila unachosikia’ jambo lillloibua furaha kwa wale wote waliokuwa na wasiwasi na ujauzito.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU