CHAPECOENSE INAVYOJIPANGA UPYA CHINI YA MANCINI

CHAPECOENSE INAVYOJIPANGA UPYA CHINI YA MANCINI

732
0
KUSHIRIKI

Chapeco, Brazil

Timu ya Chapecoense iliyokumbwa na janga la ajali ya ndege wakati wanaelekea kwenye fainali ya Copa Sudamericana, Novemba mwaka jana, wameanza tena mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka huu nchini Brazil.

Klabu hiyo iliyoibuka miaka ya hivi karibuni katika soka la Brazil, ikishika nafasi za kati za msimamo wa ligi hiyo na kutinga fainali hiyo ya Copa Sud mwaka jana.

Lakini bahati mbaya kikosi hicho kimebakisha wachezaji wanne, baada ya ajali ya ndege ya LaMia flight 2933 iliyotokea Novemba 28, mwaka jana walipokuwa wakielekea mjini Medellin nchini Colombia kucheza fainali hiyo ya kwanza dhidi ya Atletico Nacional.

Sasa ni wiki sita tangu kutokea kwa ajali hiyo, timu hiyo ya mjini Chapeco imeanza mazoezi ikiwa na kocha mpya, Vagner Mancini.

Kikosi hicho kilichoanza mazoezi kilijumuisha wachezaji wapya 15, wanne kutoka kwenye kikosi cha zamani na 10 waliopandishwa kutoka timu ya vijana

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU