KOCHA WA VIJANA KIKAPU AWAPA TANO WAZAZI

KOCHA WA VIJANA KIKAPU AWAPA TANO WAZAZI

323
0
KUSHIRIKI

NA SHARIFA MMASI

KOCHA wa mpira wa kikapu nchini, Bahati Mgunda, amewapa tano wazazi kutokana na kuwaruhusu vijana chipukizi  kujiunga na klabu mbalimbali kwa lengo la kujifunza mchezo huo.

Akizungumza na BINGWA jana,  Mgunda alisema zaidi ya wachezaji 300 chipukizi wamepita katika mikono yake na wengi wao wanaendelea kufanya vema katika michuano mbalimbali  ya kitaifa na kimataifa.

Mgunda alisema anawashukuru wazazi  kwa kuonyesha moyo wa kizalendo wa kuwaruhusu vijana wao kujiunga na klabu za mpira wa kikapu, ambao una manufaa kwa mchezaji na taifa kwa ujumla.

“Tangu nianze kufundisha vijana chipukizi namna ya kuwa wachezaji bora wa kikapu, zaidi ya vijana 300 wamepita katika mikono yangu na mpaka sasa wapo salama wanaendelea kufanya vema katika michuano ya kitaifa na kimataifa,” alisema Mgunda.

Mgunda alisema ni vema wazazi watambue kuwa mpira wa kikapu una faida kwa wachezaji, muhimu ni kuhakikisha wanawapa moyo vijana wao na kufuatilia maendeleo yao.

“Mahala popote penye maendeleo lazima pawe na nguvu zaidi ya mtu mmoja, kwa maana hiyo kocha pekee hana uwezo wa kumfanya mchezaji afikie malengo yake yote, kuna kila sababu ya wazazi kuungana na walimu katika kuhakikisha wanakwenda sambamba kutimiza ndoto za  vijana hao,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU