LUIZIO AWAOTA MABEKI WA URA

LUIZIO AWAOTA MABEKI WA URA

1067
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM, ZANZIBAR

MSHAMBULIAJI wa Simba, Juma Luizio, amewaota mabeki wa URA ya Uganda kutokana na shughuli pevu aliyoipata katika mchezo wa makundi wa Kombe la Mapinduzi, uliomalizika kwa kutoka sare tasa kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.

Akizungumza na BINGWA jana, Luizio alisema kamwe hatawasahau mabeki wa timu hiyo, ambao walikuwa ni kikwazo kwake kufunga bao katika mchezo huo uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja huo.

Luizio alisema kati ya mabeki waliokutana nao kwenye michuano hiyo wale wa URA ni kiboko kutokana na uwezo wao wa kukaba na kuzuia mashambulizi.

Alisema katika michezo minne aliyocheza kwenye michuano hiyo,  hajaona mabeki wengine waliomsumbua,  licha ya kutoka sare tasa na Yanga katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Amaan.

Luizio alisema katika timu zote walizokutana nazo mabeki wa URA walimsumbua kupita kiasi kutokana na mfumo waliokuwa wakiutumia katika mchezo wao.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU