TAMBWE ASIMULIA MWINYI ALIVYOMBANIA KUIUA SIMBA

TAMBWE ASIMULIA MWINYI ALIVYOMBANIA KUIUA SIMBA

3584
0
KUSHIRIKI
????????????????????????????????????

NA HUSSEIN OMAR

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amesimulia maumivu aliyoyapata baada ya timu yake kufungwa 4-2 kwa penalti na Simba huku akimtaja beki, Hajji Mwinyi, kwamba ndiye aliyesababisha Simba wasilale na viatu.

Katika mchezo huo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan, Mwinyi alipiga penalti ya nne ambayo iliokolewa na kipa Daniel Agyei wa Simba na kumpa nafasi Javier Bokungu, kufunga penalti ya mwisho na hivyo Yanga kushindwa kumalizia mkwaju uliobaki.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe, alisema alijipanga kupiga penalti ya nne, lakini Mwinyi akamtaka yeye awe wa mwisho ili kumaliza shughuli, hivyo yeye Tambwe alikuwa apige penalti ya tano ambayo pengine ingekuwa ya ushindi au ingeongeza matuta kwenye mchezo huo.

“Ukweli ni kwamba, nilikuwamo  kwenye orodha ya waliokuwa wanapiga penalti ila nilikuwa nipige ya tano lakini baada ya wenzangu kukosa sikubahatika kupiga, ila niseme tu hatukuwa na bahati ya ushindi na pelanti hazina mwenyewe,” alisema Tambwe.

Alisema upigaji wa penalti hauna ufundi ndio maana utaona hata wachezaji nyota duniani kama Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona, nao wanakosa hivyo hilo si jambo la kushangaza.

Katika hatua nyingine, Tambwe amewatuliza mashabiki wao akiwaambia kuwa wasife moyo kutokana na kutupwa nje kwenye michuano hiyo na badala yake wasubiri mambo mazuri Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU