YANGA KILIO KILE KILE

YANGA KILIO KILE KILE

1121
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM, ZANZIBAR

YANGA wameendelea kulia kilio kile kile cha wachezaji wao kujiamini kupita kiasi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya juzi kutolewa  katika mchezo wa nusu fainali kwa changamoto za mikwaju ya penalti 4-2  na Simba kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90, uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.

Kabla ya kutinga hatua hiyo, Yanga ilipigwa mabao 4-0 na Azam katika mchezo wa makundi, ambayo ilikuwa imeshinda michezo miwili ya awali iliyowabeba na kuvuka.

Akizungumza na BINGWA juzi visiwani hapa, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema tatizo la wachezaji mara zote ni kujiamini sana kabla ya kupata matokeo.

Mwambusi alisema sababu hiyo ndiyo iliwafanya wapoteze michezo miwili mfululizo ya Kombe la Mapinduzi, ikiwamo wa Simba ambao walitolewa kwa changamoto ya penalti.

“Tunajua wachezaji wetu wameingia kwa kujiamini sana, tumeligundua hilo na tutalifanyia kazi,” alisema Mwambusi.

Mwambusi alisema baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, wanayafanyia kazi mapungufu  yaliyojitokeza  ili waweze  kujiandaa vema na mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU