STAA JAMHURI YA CZECH AJIUA

STAA JAMHURI YA CZECH AJIUA

322
0
KUSHIRIKI

 PRAHA, Jamhuri ya Czech

SHIRIKISHO la Soka la Jamhuri ya Czech limethibitisha kuwa nyota wa kikosi cha timu ya Taifa, Frantisek Rajtoral, amejiua akiwa na umri wa miaka 31.

Hadi anajiua, kiungo huyo wa timu ya Gaziantepspor alicheza mara 19 katika michuano ya Super Lig tangu alipojiunga nayo akitokea Viktoria Plzen, ambako alishinda mataji manne ya Ligi Daraja la Kwanza ya Jamhuri ya Czech katika kipindi cha misimu nane.

Kwa upande wa timu ya taifa, aliicheza mara 14 Jamhuri ya Czech na alikuwa miongoni mwa kikosi kilichoshiriki michuano ya fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.

“Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia yote ya marehemu,” ilieleza taarifa iliyotolewa na Rais wa timu ya Gaziantepspor, Levent Kizil, kama ilivyonukuliwa na mtandao wa Sporx:

“Kwa masikitiko naweza kuthibitisha kuwa, taarifa za kujiua ni za kweli,” iliongeza taarifa hiyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU