JULIET IBRAHIM AKIRI KULA URODA UFUKWENI

JULIET IBRAHIM AKIRI KULA URODA UFUKWENI

742
0
KUSHIRIKI

LAGOS, Nigeria

STAA wa tasnia ya filamu mwenye asili ya Ghana katika kijiji cha Nollywood, Juliet Ibrahim, amekiri kuwa amekuwa akibanjua amri  ya sita katika maeneo ya wazi bila kujali watu waliomzunguka.

Staa huyo alitoa kauli hiyo hivi karibuni, katika mahojiano na kipindi kinachorushwa na Kituo cha televisheni cha Trybes TV kiitwacho On My Honour.

Katika mahojiano hayo, mwanamama huyo mwenye mtoto mmoja alisema kwamba amekuwa akifanya vitendo hivyo maeneo ya ufukweni na kwamba kila kitu kimekuwa kikienda sawia, hata kama ufukweni kuna watu wengi.

“Ni kitu kinachojitokeza tu na wala hakipangwi. Sote tunakuwa tumekwenda kuvinjari na kuna uwapo wa watalii wengi, hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kukereka,” alisema nyota huyo.

Hata hivyo, aliwashauri mashabiki wake kuwa makini watakapotaka kufanya vitendo hivyo maeneo ya pwani.

“Unatakiwa kuwa makini unapotaka kufanya hivyo. Unapotaka kufanya ama kujaribu unatakiwa kuhakikisha maeneo hayo yanaruhusiwa na si katika nchi ama eneo ambalo utatiwa hatiani,” alishauri kimwana huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU