CASSPER NYOVEST MJUKUU WA NELSON MANDELA ANAYETUA NCHINI KUMPIMA UBAVU DIAMOND

CASSPER NYOVEST MJUKUU WA NELSON MANDELA ANAYETUA NCHINI KUMPIMA UBAVU DIAMOND

610
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

JULAI 22, 2017, mkali wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, anatarajiwa kupata fursa ya kupimana ubavu na rapa nyota wa Afrika Kusini anayekwenda kwa jina la Cassper Nyovest.

Tukio hilo limepangwa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na wawili hao, pia atakuwapo rapa hatari kutoka Marekani anayefahamika kwa jina la Future.

Future ambaye jina lake kamili ni Nayvadius DeMun Wilburn, amejizolea umaarufu kede kede nchini Marekani na duniani kwa ujumla kutokana na umahiri wake aliouonyesha katika kuimba, ‘kurap’ na kuandika nyimbo zenye ubora wa hali ya juu, lakini pia akiwa amejiwekea rekodi ya kutoa albamu mbili ndani ya wiki moja ambazo zote zimebamba ‘kinoma’.

Wakati wapenzi wa muziki nchini wakionekana kusubiri kwa hamu ujio wa Future, hatimaye imetangazwa kuwa Nyovest naye atakuwapo katika tamasha hilo lililopewa jina la Castle Lite Unlock.

Nyovest ambaye jina lake kamili ni Refiloe Maele Phoolo, ni rappa aliyefanikiwa zaidi nchini Afrika Kusini ambaye amekuwa akitengeneza historia kila leo, huku akiwa haonyeshi dalili ya kupunguza mwendo.
Kikubwa zaidi ambacho alikifanya ni kuujaza Uwanja wa Orlando mwaka jana katika moja ya shoo zake, jambo ambalo halikuwa likitegemewa na watu wengi ndani ya nchi hiyo iliyotambulishwa vilivyo na mwasisi wake, hayati Nelson Mandela ambaye alipambana sana kuipigania, ikiwamo kutumikia kifungo ili watu wake waweze kupata uhuru kutoka kwa makaburu.

Katika onyesho hilo, watu 40,000 walishuhudia shoo hiyo ya kihistoria aliyoiandaa yeye mwenyewe.
Tamasha hilo alilolipa jina FillUpOrlando, lilifanyika Oktoba 30 mwaka jana na kumfanya awe si tu rappa wa kwanza, bali msanii wa Afrika Kusini wa kwanza kuwahi kuujaza uwanja huo.
Mwaka huu, Cassper ana mpango wa kuujaza Uwanja wa FNB ambao huchukua watu 80,000.

Desemba 2, mwaka jana, Kituo cha Televisheni cha MTV Base kilimweka Cassper Nyovest katika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya waimbaji bora kabisa wa Afrika Kusini kwa mwaka huo (South Africa’s Hottest MCs of 2016).
Hadi sasa, Cassper ana albamu tatu ambazo ni Tsholofelo (2014), Refiloe (2015), Thuto (2017) na kwamba mpaka kufikia Januari 13, 2016, Refiloe ilikuwa imepata hadhi ya Platinum, kwa kuuza zaidi ya nakala milioni moja.
Ni wakati mzuri huu Cassper kuja Tanzania kwa sababu tayari ana wimbo aliowahi kuufanya na Diamond uitwao My Heart. Wimbo huo ulirekodiwa mwaka jana kwenye kipindi cha Coke Studio Africa.

Diamond na rappa huyo wanatarajiwa kuutumbuiza pamoja wimbo huo Leaders Club Julai 22, kwenye Castle Lite Unlock. Hiyo itakuwa mara ya kwanza Cassper kutumbuiza nchini Tanzania.

Juu ya tamasha hilo la Castle Lite Unlock, Meneja Masoko wa TBL Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe, anasema kuwa litawahusisha wasanii wengine wa hapa nyumbani ili kunogesha tukio hilo kubwa na la aina yake ya burudani.

Anasema tamasha hilo limelenga kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja kupitia tukio hilo kubwa la burudani.

“Uzinduzi huu utafikia kilele chake tarehe 22 Julai mwaka huu ambapo kutakuwa na tamasha kubwa Dar es Salaam litakalowapa nafasi wateja wetu kushuhudia wanamuziki wakubwa wa ndani na nje ya nchi, hivyo kuwapa wateja burudani itakayokuwa kwenye kumbukumbu zao kwa muda mrefu,” alisema Kavishe.

Kavishe anaongeza kuwa kwa kipindi chote cha kampeni hiyo, zawadi kedekede zitatolewa zikiwamo muda wa maongezi wa simu za mkononi wa zaidi ya milioni 30 na pia tiketi zaidi ya elfu moja kwa washindi wa droo ambazo zitakuwa zinashindanishwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Afrika Mashariki, Thomas Kamphius, anasema: “Kampeni ya ‘Castle Lite Unlocks’ imekuwa kwenye harakati za maandalizi kwa miaka michache sasa, ambapo Castle Lite imebadili mfumo wa kawaida uliozoeleka kwa kuwaletea wasanii wa ngazi ya juu kimataifa ili kuburudisha  ukanda wa Pwani ya Afrika kwa maonesho yaliyo na uzoefu wa ‘Extra Cold katika kilele cha tamasha ‘Castle Lite Unlocks’, anasema Kamphius.

Anaongeza: “Tunaelewa kwamba wateja wetu si kila mara wanapata fursa ya kuona baadhi ya matukio haya makubwa, hivyo tunataka kuwaletea fursa hii na kuendelea  kuwaletea uhalisia wa kukumbukwa na mara moja katika uzoefu wa tukio.”

Hali ya baadaye ya muziki inaonekana ni shwari ya kisasa  na inayohusiana na ipo njiani  kujenga  baadhi ya chapa binafsi zilizo imara, ambao unafungamana na huko nyuma na michakato ambayo ndio tunahusika nayo kwa ujumla,” Kamphius aliongeza.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU