FAINALI TATU, REKODI MBILI NGUMU KWA ZINEDINE ZIDANE

FAINALI TATU, REKODI MBILI NGUMU KWA ZINEDINE ZIDANE

682
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania

JUNI 3, mwaka huu pale jijini Cardiff, Real Madrid na Juventus, timu ambayo Zinedine Zidane aliwahi kuitumikia kwa zaidi ya miaka 10, zitachuana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kabla ya mtanange huo, Los Blancos watakabiliwa na fainali tatu za La Liga dhidi ya Celta Vigo, Malaga na nyingine waliyoicheza usiku wa kuamkia jana dhidi ya Sevilla; ushindi kwa takribani mechi zote utamfanya Zidane afikishe rekodi mbili ngumu.

Kwanini ni rekodi ngumu? Madrid haijawahi kushangilia mataji mawili mfululizo ya Ulaya tangu mwaka 1958, mwaka ambao walinyakua taji lao la tatu la Ulaya.

Wakabeba tena miaka iliyofuatia ya 1959, 1960 na 1966 enzi hizo likiitwa Kombe la Ulaya na miaka ya 1998, 2000, 2002, 2014 na 2016 likiitwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Makombe yote hayo waliyatwaa moja moja na kila msimu walipochukua taji hilo, hawakuweza kubeba na La Liga kwa wakati mmoja.

Rekodi nyingine ‘isiyowezekana’ kuwekwa na Zidane pamoja na kikosi chake ni kuwa timu ya kwanza kunyakua mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tangu mfumo na jina la michuano lilipobadilishwa mwaka 1993, hakuna timu iliyofanikiwa kufanya hivyo.

AC Milan na Juventus zilikaribia kuweka rekodi lakini zikashindwa.

Na kama unadhani ni rekodi nyepesi kuwekwa, Barcelona ya Lionel Messi ilishindwa hata kucheza fainali mbili mfululizo za Ulaya.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU