KILA LA HERI SERENGETI BOYS

KILA LA HERI SERENGETI BOYS

312
0
KUSHIRIKI

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys), leo inashuka dimbani kutupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana wa umri huo huko nchini Gabon.

Serengeti Boys inashiriki fainali za michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Tanzania kufuzu kwenye michuano hiyo na kuweka historia  katika soka la vijana hapa nchini.

Timu hiyo iko chini ya kocha wake Bakari Shime pamoja na mshauri wa ufundi wa timu za vijana, Kim Poulsen, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ayoub Nyenzi, kocha wa makipa Mohamed Muharami, daktari wa timu, Shecky Mngazija na mtunza vifaa, Edward Edward.

Seringeti Boys inaanza safari yake ya michuano hiyo kwa kumenyana na mabingwa watetezi Mali kabla ya kukabiliana na Angola siku ya Alhamisi, Mei 18 na hatimaye Niger siku ya Jumapili, Mei 21.

BINGWA tunaitakia kila la heri timu hiyo katika michuano hiyo ambayo tunaamini pamoja na mambo mengine itatoa nafasi kwa wachezaji wetu kujitangaza na kuitangaza Tanzania katika soka la kimataifa.

Watanzania wapenda soka wote wako nyuma ya timu hiyo na tunaomba kila mdau wa soka afanye sala kuiombea timu hiyo ili ipate ushindi katika mechi mbili utakaoiwezesha timu hiyo kucheza nusu fainali na hatimaye kufuzu kwa Kombe la Dunia la vijana baadaye mwaka huu nchini India.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU