DAVIDO AKACHA VIPIMO VYA DNA

DAVIDO AKACHA VIPIMO VYA DNA

664
0
KUSHIRIKI

LAGOS, Nigeria

MWIMBAJI mahiri na mtoto wa bilionea, David Adeleke, maarufu kama ‘Davido’, anaripotiwa kukacha kufanyiwa kipimo cha vina saba (DNA) ili kuthibitisha kama mtoto wa tatu ni wa kwake.

Siku chache zilizopita, Davido alipata mtoto wake wa pili wa kike aliyempa jina la Hailey, baada ya wa kwanza anayeitwa Amanda.

Hata hivyo, pamoja na kuwa na watoto hao wawili, kuna mwanamke anayeitwa Ayomide Labinjo, ambaye anamshutumu mwimbaji huyo kwa kumpa ujauzito miaka mitatu iliyopita na akatelekeza majukumu kama baba.

Hata hivyo, kinara huyo kwa mara kadhaa amekuwa akimkana mtoto huyo hadharani na tangu kipindi hicho, Labinjo amekuwa akimtaka wakafanye vipimo vya DNA, lakini staa huyo amekuwa akichomoa.

Kutokana na mvutano huo, katika mahojiano na mtandao wa Punch, mwanamama huyo alimshangaa Davido ni kwa nini anawajali watoto wale wawili, lakini anakataa kufanya hivyo kwa mtoto wake huyo aitwaye Mitchell, ambaye anadai ndiye wa kwanza.

“Wakili wetu alimtumia barua baba yake Davido tangu Aprili 20, 2017, lakini hadi sasa hatujapata majibu. Sifurahishwi na hali hiyo,” alisema mwanamama huyo.

“Ni kitu kitakachonifurahisha kwa Davido? Ni lazima achukue jukumu la kulea mtoto wake, Mitchell kama anavyofanya kwa Imade na ninafahamu fika ni jinsi gani atakavyofanya kwa huyo mwingine. Kwa nini liwe jukumu langu peke yangu,” alihoji kwa kubwata mwanamama huyo.

Alipohojiwa kuhusu jinsi staa huyo anavyofanya ni wazi huyo si mtoto wake, mrembo huyo alidai kuwa, kama anabisha ajitokeze wakafanye kipimo kingine cha DNA.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU