AZAM FC WATAFAKARI UPYA WALIPOJICHANGANYA

AZAM FC WATAFAKARI UPYA WALIPOJICHANGANYA

501
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM,

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajia kumalizika mwishoni mwa wikiendi hii, Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba, amepewa jukumu la kusuka mipango mipya kwa ajili ya msimu ujao.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya timu hiyo msimu huu kutofanya vizuri na kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kukosa nafasi kwenye Ligi Kuu na Kombe la FA.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Nassor Idrissa ‘Father’, ameliambia BINGWA  kwamba kitendo cha kupoteza nafasi hizo bodi ya wakurugezi ya Azam imeamua kumwachia majukumu kocha huyo ili kuhakikisha msimu ujao hayajirudii makosa tena.

“Suala la usajili kwa sasa hatutaki kukurupuka, tunasubiri ripoti ya mwisho kutoka kwa Cioaba na kuangalia nani anakatwa na wanaondelea, hili jambo litafanyika mapema kabla ya kocha huyo kwenda mapumziko,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU