DOGO MFAUME KUZIKWA LEO CHANIKA

DOGO MFAUME KUZIKWA LEO CHANIKA

554
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO,

MSANII wa Bongo Fleva, Mfaume Selemani ‘Dogo Mfaume’ aliyetamba zaidi na wimbo wa Kazi ya Dukani, anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Chanika, jijini Dar es Salaam.

Dogo Mfaume, aliyekuwa akipatiwa matibabu ya matumizi ya madawa ya kulevya (Sober House) alifarika jana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kichwani.

Akizungumza na BINGWA, Kaka wa marehemu, Isihaka Salehe, amesema mwili wa Dogo Mfaume utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele saa saba mchana kwenye makaburi ya Mbiki, yaliyopo Chanika, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

“Tunawashukuru wote waliokuwa nasi kipindi hiki, tunawashukuru sana, leo marehemu atapumzishwa rasmi kwenye nyumba yake ya milele saa saba mchana,” alisema.

Dogo Mfaume amefariki jana Hospitali ya Muhimbili wakati akisubiri Ijumaa (leo) ili aweze kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kichwani.

Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU