HIVI NDIVYO LIGUE 2 ITAKAVYOKWISHA KI-AJABU

HIVI NDIVYO LIGUE 2 ITAKAVYOKWISHA KI-AJABU

1498
0
KUSHIRIKI

PARIS, Ufaransa

SAHAU kuhusu vita ya kuwania ‘top four’ baina ya timu mbili za Ligi Kuu England; Arsenal na Liverpool, ambao mechi zao zitakuwa na presha, kuna Ligue 2 ya huko Ufaransa, ambayo ina timu sita ambazo zimeshikana mashati kuwania taji hadi mechi ya kumaliza msimu.

Hiyo ni ligi ya pili baada ya ile Ligue 1, na timu hizo zimepishana kwa tofauti ya pointi tatu, huku kila mechi ikibaki moja kwa kila timu.

Na mechi zote zitapigwa leo.

Baada ya miezi tisa na mechi 37, Strasbourg, Amiens, Troyes, Lens, Brest na Nimes zote zimekamatana mashati kuliwania taji la ligi hiyo, sambamba na nafasi za kupanda Ligue 1.

Strasbourg ndio vinara wakiwa na pointi 64, huku Amiens na Troyes wakifuatia na pointi 63.

Lens na Brest wako chini yao wakiwa na pointi 62, Nimes akimaliza ‘top six’ hiyo na pointi 61.

Klabu mbili tu ndizo zitakazopata nafasi ya kupanda daraja moja kwa moja, huku ile ya tatu ikitakiwa kucheza ‘play-off’.

Sasa basi, huu ndio ufafanuzi wa bingwa atakavyopatikana leo:

Mosi, Strasbourg inahitaji kushinda mechi yao ili kuwaacha wapinzani wake wote watano kwenye mataa.

Hata hivyo, kama Amiens akishinda na Strasbourg akafungwa au kutoa sare, basi wataubeba ubingwa wao.

Amiens pia wanaweza kubeba taji kama Strasbourg atapoteza pointi na timu zote zilizo chini yao zikashindwa kupata ushindi kwenye mechi zao.

Matumaini ya Troyes kubeba taji yatategemea kuziona Strasbourg na Amiens zikifungwa au kutoa sare, kwani tofauti yao ya mabao hairidhishi.

Lens watabeba kombe hilo iwapo watapata ushindi na kuziombea mabaya timu tatu za juu zipoteze pointi.

Wakati huo huo, Brest na Nimes zitategemea timu za juu zote zifungwe ili mmojawapo abebe ubingwa.

Huu ndio utamu wa soka bwana!

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU