MALAIKA: WAZAZI WAHESHIMU NDOTO ZA WATOTO

MALAIKA: WAZAZI WAHESHIMU NDOTO ZA WATOTO

567
0
KUSHIRIKI

Na JOHANES RESPICHIUS,

STAA wa singo ya Rarua Rarua, Diana Exavery ‘Malaika’,  amewataka wazazi kuheshimu ndoto za watoto wao na kuacha kulazimisha wafuate matakwa yao.

Malaika, ambaye anatarajia kuhamishia makazi yake nchini Uingereza, aliyasema hayo juzi, alipotembelea ofisi za gazeti hili, huku akisisitiza uwepo wa wazazi ambao wamekuwa wakikwamisha ndoto za watoto wao kwa mtindo huo wa kuwalazimisha.

“Nimekuja kuelewana na kukaa meza moja na baba yangu mzazi baada ya Rais Dk. John Magufuli kusema kuwa, mimi ni miongoni mwa wasanii anaowakubali, kwani alikuwa amenisusa kutokana na kunizuia kufanya muziki bila mafanikio,” alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kusikia ametajwa na Rais, ndipo mzee wake alipompigia simu na kutaka wayaongee.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU