MGANDA: NGOMA YENYE HESHIMA KUBWA KWA WANYASA NA WANGONI

MGANDA: NGOMA YENYE HESHIMA KUBWA KWA WANYASA NA WANGONI

1003
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE,

Mganda-Ni ngoma ya kabila la Wangoni na Wanyasa mjini Songea na kandokando ya Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Ngoma hii inapendwa na ina heshima kubwa kwa watu wa eneo hilo.

Huchezwa kipindi cha furaha, kumtambulisha mtemi mpya au kukiwa na ushindi wowote, mavuno, harusi pamoja na kipindi ambacho vijana wanatoka jando.

Ngoma hii huchezwa kwa staili tofauti kulingana na wimbo au maudhui ya sherehe, lakini hautofautiana kutokana na aina ya nguo wanazovaa. Huvaa kaptula, shati, soksi vyote vya rangi nyeupe ila mkanda na viatu ndio huwa vyeusi na kama watavaa kofia hasa kwa wale wanaocheza mganda wa kipingi basi itakuwa nyeupe.

Mara zote ngoma hii huchezwa na wanaume pekee na inapochezwa vyakula vya asili na pombe hupikwa. Kwa sasa ni moja ya ngoma zinazopendwa sana hapa nchini.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU