MSUVA, MANULA KUKOMBA MAMILIONI YA SIMBA

MSUVA, MANULA KUKOMBA MAMILIONI YA SIMBA

3065
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

MLINDA mlango wa Azam FC, Aishi Manula na winga wa Yanga, Simon Msuva, huenda wakakomba mamilioni ya Simba waliopewa na wadhamini wao wapya, kama klabu hiyo ya Msimbazi itasikiliza ushauiri wa beki wao wa kulia, Janvier Besala Bokungu ambaye anatamani wachezaji hao watue kwenye timu yake hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Beki huyo wa DR Congo, Bokungu amewataja wachezaji kuwa ni nyota wanaomvutia na anatamani klabu yake ingefanya mpango wa kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wachezaji hao aliowataja pia wamo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliotajwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juzi, pia amemtaja mkali wa mabao wa Kagera Sugar, Mbaraka Yussuph ambaye naye yuko katika orodha ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora msimu huu.

Bukungu amesema wachezaji hao ndio ambao anaona wametoa upinzani mkubwa kwao na kwake wakati timu zao zilipokutana kwenye msimu huu wa ligi kuu.

“Kwa kweli sijafuatilia sana ila hadi sasa sijaona mchezaji kama Msuva, Manula, Mbaraka na Mohamed Samatta (Tanzania Prisons) kwa upande wa wapinzani tuliokutana nao. Natamani klabu yangu ingewasajili nicheze nao timu moja,” alisema beki huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU