UMEWAHI KUONA KIBAO KATA WEWE? NENDA JAHAZI

UMEWAHI KUONA KIBAO KATA WEWE? NENDA JAHAZI

953
0
KUSHIRIKI

NA BEATRICE KAIZA,

HAIYA Haiaaaaaah! Ule muda wa kula bata kwa kwenda mbele muda ndio huoooo umewadia kwani ni mwendo wa kula bata hadi kuku waone wivu.

Ijumaa hii hadi Jumapili  unaweza kutoka na familia, washikaji au watu wako wa karibu ili kukonga nyoyo na kupata burudani mbalimbali. Mashabiki na wapenzi wa kipande hiki twende sawa ili kujua ni viwanja gani vitapendeza wikiendi hii.

HII NI KWA MAPOPO

Kama kawa pande hizi tunarekebishana, kuonyana na kuvunjana mbavu kwa mbaali. Hivi mnajua kwamba msimu wa Ramadhani unakaribia basi wapenda bata wenzangu mnatakiwa kufanya bata la kistaarabu ili kukaribisha msimu huu kwa tabia njema.

Club Element (Masaki)

Ijumaa ni disco muziki mnene na dj Sinyolita.

Escape One (Mikocheni)

Kama wewe ni mdau wa Kareoke basi dondoka pande hii siku ya Ijumaa, maana itakuwa ni karaoke Night, kabla Skylight kumalizia Jumamosi.

WAZEE WA BAND & TAARAB

Travertine Hotel (Magomeni)

Jahazi Modern Taarab watakonga nyoyo za mashabiki wao Jumapili wakisindikizwa na mkali wa kibao kata, Kivulande na wasanii wengine kibao unakosaje kwa mfano.

Dar Live (Mbagala)

Jumapili kutakuwa na Manchester Band

Twanga Pepeta

Wazee wa kutwanga na kupepeta Jumamosi hii watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Mango Garden na Jumapili ni Toroka Uje, Kimara.

MOVIES

MLIMANI CITY

Kwa wale wapenzi wa ‘movies’, hapa kutakuwa na movie kali na wajanja wote wa jiji wanakutana hapa, cha kufanya  kamatia 3D yako ili kuweza kutazama kwa ukaribu.

Alien Covenant, Bay Watch, Meri Pyaari Bindu, Half Girlfriend, The Boss Baby.

Hizo ndizo movies ambazo zitakuwa hewani pande hizi za Mlimani City.

Imeandaliwa na Beatrice Kaiza, kama una kiwanja chako na unataka wadau wajue nini kinatokea maeneo yako, kamatia simu kisha tuma ratiba katika namba hii 0626 664 991 tu usipige simu  maana hapa bata tu hainaga kuchagua.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU