CITY YAKAMILISHA DILI LA KIPA MPYA

CITY YAKAMILISHA DILI LA KIPA MPYA

492
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester City jana imekamilisha dili la kumsajili mlinda mlango wa Brazil, Ederson, kutoka Benfica kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England.

City haikuweka wazi kuhusu ada ya uhamisho lakini vyombo vya habari vimemkadiria kipa huyo kuwa ana thamani ya pauni milioni 34.7 (dola milioni 44.92), ikiwa ni rekodi ya kiasi kikubwa cha fedha kutumika kwa kipa.

Ederson anakuwa Mbrazil wa nne kuwemo ndani ya timu hiyo sambamba na Fernandinho, Fernando na straika mahiri, Gabriel Jesus.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU