HII NDIYO SIRI YA 4:44 YA JAY Z

HII NDIYO SIRI YA 4:44 YA JAY Z

797
0
KUSHIRIKI

LOS ANGELES, Marekani

Tetesi zimezagaa kwamba rapa Jay Z anatarajiwa kuachia albamu mpya. Lakini kinachowashangaza wengi ni jina la albamua hiyo, ambalo ni 4:44.

Baada ya kuwamo kwa uvumi mwingi kwenye mitandao ya kijamii, sasa ni kama tetesi hizo zimezidi kuongezwa nguvu, baada ya DJ Booth kuandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter kwamba rapa huyo ataachia albamu hiyo ya 4:44.

Katika maelezo yake, jina hilo la albamu liliandikwa Kirumi, lakini baadaye alifuta maelezo hayo.

Kwa miezi kadhaa, tetesi zilivuma kwenye mitandao kwamba ‘Hova’ anaandaa albamu mpya, lakini mpaka sasa hakuna taarifa kamili kutoka kwa Jay Z wala kwa watu wake wa karibu kuhusu kuachiwa kwa albamu hiyo mpya, lakini imeonekana kama jambo hilo linaweza kuwa kweli, baada ya Dj Booth kuandika kwenye mtandao wake wa kijamii.

Ikiwa rapa huyo akitoa albamu hiyo ya 4:44, basi itakuwa ni mzigo wake wa 13 tangu aanze kujihusishwa na masula ya muziki.

Mwaka 2011, mke wa rapa huyo, Beyonce aliachia albamu iitwayo 4. Pia wawili hao walioana Aprili 4 (4/4) na kila mmoja ana ‘tattoo’ ya ‘IV’.

Pia inasemekana jina la kati la mtoto wao Blue Ivy, linafanana na namba ya Kirumi IV. Beyonce alizaliwa Septemba 4, naye Jay alizaliwa Desemba 4.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU