IBF WARUHUSU PAMBANO LA JOSHUA NA KLITSCHKO KURUDIWA

IBF WARUHUSU PAMBANO LA JOSHUA NA KLITSCHKO KURUDIWA

403
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

HATIMAYE Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limeruhusu kurudiwa kwa pambano la Anthony Joshua ‘AJ’ na Wladimir Klitschko.

AJ ameruhusiwa na IBF kuzichapa tena na Klitschko, lakini pambano hilo litapaswa kuchezwa kabla ya Desemba 2, mwaka huu.

Promota wa AJ, Eddie Hearn kupitia kampuni ya Matchroom Boxing, walipeleka maombi maalumu na IBF wametoa kibali.

Shirikisho hilo la ngumi limesema mshindi wa pambano hilo kati ya Joshua na Klitschko lazima akutane na Kubrat Pulev.

IBF wamesema hakutakuwa na ngumi kabla ya Desemba 2, mwaka huu na Pulev amekubaliana na sharti hilo la kusubiri marudiano ya pambano hilo la Klitschko na AJ.

Baadhi ya viwanja vimeanza kutajwa kwa ajili ya pambano hilo la marudiano kati ya Joshua na Klitschko, ambao walizipiga Aprili mwaka huu kwenye Uwanja wa Wembley.

“Tumepata ofa nyingi sana za ukumbi wa pambano hilo la marudiano, kama Nigeria, Dubai, Marekani na pia kuna nafasi Uwanja wa Cardiff (uwanja uliochezewa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu),” alisema Hearn, akizungumza na Sky Sports.

“Kifedha, Cardiff si sehemu nzuri, lakini kama uwanja hautavunja rekodi ya pambano la kwanza, ni bora msiutumie, hayo ndiyo mawazo yetu mimi na AJ katika kuhakikisha tunasonga mbele.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU