ZIJUE TAKWIMU ZINAZOMPA JEURI ZIDANE

ZIJUE TAKWIMU ZINAZOMPA JEURI ZIDANE

681
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania

BAADA ya Real Madrid kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha Zinedine Zidane ndiye anayetajwa kuwa nyuma ya mafanikio hayo. Ni kweli?

Madrid wameshinda michuano hiyo mara nane tangu mwaka 1958 na kwa mara ya mwisho ilikuwa ni wiki chache zilizopita mbele ya Juventus pale  Cardiff, Wales.

Hata hivyo, katika idadi hiyo ni msimu huu pekee ambapo Madrid wameweza kulibeba huku wakiwa mabingwa wa La Liga. Haijawahi kutokea.

Wakati Madrid walipotwaa taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2002 kwa kuichapa Bayer Leverkusen, Valencia ndiyo waliokuwa mabingwa wa La Liga.

Mwaka 2000, Madrid walichukua ubingwa wa mashindano hayo lakini walimaliza ligi wakiwa nafasi ya tano, huku Deportivo La Coruna wakibeba ndoo ya La Liga.

Hata walipoichakaza Eintracht Frankfurt mabao 7-3 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1960, Madrid waliangukia nafasi ya pili La Liga.

Miaka miwili kabla ya mchezo huo, yaani mwaka 1958, ndio uliokuwa mwisho wa Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga katika msimu mmoja.

Msimu uliomalizika, Madrid haikufunga mabao katika mchezo mmoja, walikuwa ni Borussia Dortmund ndio waliofanya hivyo. Lakini pia, hawakuruhusu mabao mengi katika mchezo mmoja. Ni FC Copenhagen ndio waliokuwa na rekodi hiyo.

Pia, hawakumaliza mechi za makundi wakiwa kileleni na badala yake walikuwa nyuma ya Dortmund, lakini msimu ujao watakuwa wakitetea mataji mawili makubwa; La Liga na Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, ikiwa na ‘Zizou’ kwenye benchi la ufundi, Madrid ndio timu iliyoshinda mechi nyingi katika msimu uliopita wa La Liga.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU