AJIB AWALIZA MSIMBAZI

AJIB AWALIZA MSIMBAZI

3932
0
KUSHIRIKI

NA ZAITUNI KIBWANA

SIKU moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib amekubaliana na matajiri wa Yanga kutua kwenye klabu hiyo ya Jangwani kwa mkataba wa miaka miwili, shabiki wa Wekundu wa Msimbazi ameshindwa kujizuia na kuangua kilio hadharani.

Tukio hilo lilitokea jana karibu na makao makuu ya klabu ya Simba, ambapo shabiki Faraja Ismail aliamua kumwaga machozi mara baada ya kuendelea uvumi kuwa straika huyo ni mali ya Yanga.

BINGWA lilishuhudia tukio hilo, ambapo Ismail alilia kwa uchungu kwa kusema kuwa wanachowafanyia Yanga kamwe hakikubaliki, ukizingatia Ajib ni mchezaji aliyelelewa kwa mapenzi makubwa ndani ya klabu hiyo.

“Niacheni tu, hivi Ajib anakwendaje Yanga na sisi tupo na tumemlea mpaka kufika hapa, wanachotufanyia Yanga hakika hakikubaliki na viongozi wajue tumeumia sana kwenye hili,” alilalama shabiki huyo, huku akijifuta machozi.

Shabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Patrick Gerad, naye alisema viongozi wa Simba sasa wanapaswa kujifunza kutoka kwa Yanga na si kukubali kila siku kuonewa tena kwa wachezaji wao muhimu.

“Walianza kwa Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Amis Tambwe na sasa Ajib, hii sasa ‘too much’,  tunapaswa kujifunza, hatuwezi kila siku kukubali kuonewa na mahasimu wetu kirahisi rahisi hivi,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU