HANSPOPE AMALIZA HASIRA ZA AJIB KWA OKWI

HANSPOPE AMALIZA HASIRA ZA AJIB KWA OKWI

3872
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

HATIMAYE Simba sasa wana uhakika wa kumtumia mshambuliaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope, kupanda ndege na kumfuata kwao Uganda na kumalizana naye kila kitu.

Ili kuthibitisha kwamba jambo hilo ni la kweli, kiongozi huyo alitupia picha akiwa na Okwi huko Uganda, hiyo ikiashiria mambo yamekwenda kama wenyewe walivyokuwa wakitaka.

Kumalizana huko na Okwi, angalau kunaweza kukawafuta machozi mashabiki wa Simba ambao wamekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kusikia kuwa kipenzi chao Ibrahim Ajib, amesaini Yanga.

Mashabiki hao wa Simba, wamejikuta wakipatwa na butwaa baada ya kuenea taarifa hizo za Ajib kusaini Yanga lakini sasa wanaweza kushusha presha baada ya uongozi wao kumpandia ndege Okwi, ambaye ana rekodi nzuri ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Kigogo mmoja wa Simba amelithibitishia BINGWA kwamba picha zile alizopiga Hanspope na Okwi, ni tukio lililofanyika nchini Uganda ambapo mwenyekiti huyo wa usajili alikwenda kuweka mambo sawa.

“Ni kweli Hanspope amekwenda kule na hizo picha mnazoziona akiwa na Okwi ni za kweli, kwani walikutana huko na kila kitu kimekwenda sawa,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU