KABUNDA KULAMBA MKATABA MPYA MWADUI

KABUNDA KULAMBA MKATABA MPYA MWADUI

1040
0
KUSHIRIKI

NA ESTHER GEORGE

WINGA wa kushoto wa Mwadui FC, Hassan Kabunda, yupo kwenye mazungumzo ya mwisho ili kuongeza mkataba wa kuitumikia timu hiyo yenye makao yake makuu Mwadui, Shinyanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhani Kilao, alisema mazungumzo kati ya pande hizo mbili yako kwenye hatua nzuri na huenda mchezaji huyo akaendelea kuichezea timu yao.

“Kabunda ni mchezaji wetu mwenye uwezo mzuri tu na tunafanyia kazi maombi yake ya kuomba aongezewe mkataba, hivyo wakati wowote tutatoa tamko rasmi,” alisema Kilao.

Hata hivyo, alisema klabu yake bado haijaanza rasmi zoezi la usajili kwaajili ya msimu ujao.

“Ripoti ya kocha inaonyesha anahitaji wachezaji wanne, washambuliaji wawili na viungo wawili, hata hivyo, zoezi la usajili bado hatujalianza kwakuwa hatuna haraka,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU