YANGA WAMWACHA NJIAPANDA BARTHEZ

YANGA WAMWACHA NJIAPANDA BARTHEZ

1746
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

UONGOZI wa Yanga umemweka njiapanda kipa wa timu hiyo, Ally Mustapha `Barthez`, kutokana na hatua yao ya kutomweleza chochote kama utaendelea naye au utaachana naye.

Yanga inadaiwa kutokuwa na nia ya kumwongezea mkataba Barthez na badala yake unahusishwa na mpango wa  kumsajili aliyekuwa kipa wa timu ya African Lyon, Youthe Rostand.

Barthez ameliambia BINGWA jijini jana kuwa, hadi sasa hajui hatima yake Yanga, kutokana na uongozi wa klabu hiyo kutomweka wazi kuhusiana na majaliwa yake.

Alisema anachokisubiri kwa sasa ni taarifa rasmi kutoka kwa mabosi zake hao, kama anaondoka Yanga au anaendelea kusalia kwa msimu mwingine.

“Nina mkataba wa mwaka mmoja, hivyo sitaweza kuingia katika mazungumzo na timu nyingine, hadi nitakapopewa barua yangu ya kuachwa rasmi na Yanga,” alisema Barthez.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU