KIUNGO MPYA YANGA ATAKA UZI NAMBA TATU

KIUNGO MPYA YANGA ATAKA UZI NAMBA TATU

2934
0
KUSHIRIKI

NA SALMA MPELI

KIUNGO mpya wa Yanga, Pius Buswita, amesema anahitaji kuvaa jezi namba tatu inayovaliwa na beki wa timu hiyo, Oscar Joshua, katika mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine.

Akizungumza na BINGWA jana,  Buswita alisema angependa kuvaa jezi hiyo akiwa na kikosi hicho cha Jangwani.

“Naipenda jezi namba tatu na ndiyo jezi niliyokuwa naitumia siku zote hivyo ningependa kwenye kikosi cha Yanga nivae jezi hiyo,” alisema Buswita.

Buswita alisema amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano na Yanga.

Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Yanga ni Abdallah Haji ‘Ninja’ wa Jang’ombe Boys ya Zanzibar na Gadiel Michael (Azam) Ibrahim Ajib (Simba).

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU