MURRAY KUVAANA NA ‘NDUGU YAKE’ RAUNDI YA KWANZA YA AEGON

MURRAY KUVAANA NA ‘NDUGU YAKE’ RAUNDI YA KWANZA YA AEGON

387
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

MKALI wa tenisi, Andy Murray, anatarajia kukutana na Mwingereza mwenzake, Aljaz Bedene, kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya tenisi ya Aegon katika Uwanja wa Queen’s Club kesho.

Nyota hao wanakumbukwa kwa pambano lao la mwaka jana ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Murray, alimchakaza Bedene kwa seti mfululizo.

Mkali kutoka Uswisi, Stan Wawrinka, amepangiwa kuoneshana kazi na Mhispania, Feliciano Lopez, wakati Nick Kyrgios wa Australia akitarajia kuvaana na Steve Johnson wa Marekani.

Sam Querrey ambaye aliibuka bingwa wa mashindano hayo mwaka 2010, atachuana na Mwingereza, Cameron Norrie, huku Mcanada Milos Raonic ambaye alitinga fainali mwaka jana akikabiliwa na jukumu zito dhidi ya Thanasi Kokkinakis wa Australia.

Mashindano hayo yanatazamiwa kama ngazi kwa wachezaji wa kiume wanaoongoza kwa viwango kuelekea michuano ya Wimbledon, ambapo hadi sasa wakali wa 20 bora kwenye mashindano ya Aegon wapo 10.

“Mashindano ya mwaka huu yatakuwa magumu kutokana na aina ya wachezaji waliopo,” alisema Kyrgios.

“Ni maandalizi mazuri kwetu kuelekea Wimbledon. Mashindano haya nimekuwa nikiyatazama kwa jicho makini hasa kwenye uwanja wa nyasi,” aliongeza.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza leo hadi Juni 25 mwaka huu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU