NYAMLANI AKOLEZA JOTO UCHAGUZI TFF

NYAMLANI AKOLEZA JOTO UCHAGUZI TFF

654
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, amejitosa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika Agosti 12, mkoani Dodoma.

Nyamlani alichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo jana saa 12 mchana katika Ofisi ya shirikisho hilo jijini Dar es Salaam, akifuatiwa na Fredrick Mwakalebela.

Katika uchaguzi uliopita uliofanyika Oktoba mwaka 2013, kwenye Ukumbi wa Water Front jijini  Dar es Salaam,  Nyamlani aliwania nafasi hiyo lakini aliangushwa na  Jamal Malinzi  aliyejitokeza kutetea nafasi yake.

Nyamlani ambaye ana uzoefu katika masuala ya uongozi wa soka, amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika utawala wa Rais Leodegar Tenga aliyemwachia kijiti Malinzi.

Lakini wamewahi kushika nafasi nyingine katika uongozi wa soka, akiwa Ofisa Tawala wa FAT chini ya mwenyekiti Subira Mambo, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kile cha Wilaya ya Temeke (TEFA).

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Nyamlani alisema ameamua kuwania nafasi hiyo kwa kuwa ana sifa  zote za kuongoza mpira.

Nyamlani alisema katika uchaguzi uliopita, aliwania lakini kura hazikutosha na ameamua kujitosa kwenye uchaguzi ujao.

Wengine waliojitokeza kuwania nafasi ya urais ni pamoja na Imani Madega,  Wallace Karia, Fredrick Masolwa.

Kwa nafasi za umakamu wa urais waliochukua fomu tayari  ni Mulamu Nghambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange.

Katika nafasi ya Kamati ya Utendaji ni  Salum Chama, Ephraim Majige, Elias Mwanjala, Saleh Alawi, Kaliro Samson, Vedastus Lufano, Kenneth Pesambili, Mbasha Matutu, Samuel Daniel, Dunstan Mkundi, Athumani Kambi, Shaffi Dauda, Golden Sanga, Charles Mwakambaya, Benista Rugola, Thabit Kandoro na Goodluck Moshi.

Wengine ni James Mhagama, Hussein Mwamba, Sarah Chao, Issa Bukuku, Stewart Masima, Emmanuel Ashery, Abdul Sauko, Mussa Sima, Stanslaus Nyongo, Ayoub Nyenzi, John Kadutu, Baraka Mazengo, Khalid Mohamed, Mohamed Aden, Cyprian Kuyava na Saleh Abdul, Omar  Ally, Lameck Nyambaya, Abdallah Mussa, Ally Mussa, Peter Mhinzi, Said Tully na Mussa Kisoki.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU