STRAIKA MWINGINE KUSAINI MIAKA MIWILI YANGA

STRAIKA MWINGINE KUSAINI MIAKA MIWILI YANGA

3134
0
KUSHIRIKI

NA MARTIN MAZUGWA

BAADA ya Yanga kunasa saini ya  Ibrahim Ajib, straika mwingine Rafael Daud kutoka Mbeya City anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili  baada ya kumaliza kuitumikia Simba aliyoichezea kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha timu yake kuchukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho hivi karibuni.

Yanga wanatarajia kumalizana na Daud baada ya  kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo kwa dau la Sh milioni 30 kwa ajili ya msimu ujao.

Daud ambaye alikuwa anawaniwa na Singida United, anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam  kukamilisha usajili akitokea kwao mkoani Singida ambako alikwenda kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Daud alisema pamoja na dau atakalopewa, lakini atapangiwa nyumba na mshahara monono atakaolipwa kila mwezi.

“Ninachosubiri hivi sasa ni kutumiwa nauli ili niweze kwenda Dar es Salaam kumalizana na Yanga, kwani tumekubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili,” alisema Daud.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU