STRAIKA NDANDA ANUKIA JANGWANI

STRAIKA NDANDA ANUKIA JANGWANI

2577
0
KUSHIRIKI

NA MARTIN MAZUGWA

STRAIKA wa Ndanda, Omari Mponda, amesema yupo mbioni kujiunga na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Yanga kama dili lake litakamilika.

Katika msimu uliopita, Mponda  alionekana kuzisumbua Simba na Yanga  ambapo alimaliza akiwa ameifungia klabu yake mabao sita.

Akizungumza na BINGWA jana, Mponda alisema kwa sasa bado anaendelea na mazungumzo na Yanga na mambo yakienda sawa atamwaga wino  kwa kuitumikia katika mismu miwili.

“Sikuwa sawa mzunguko wa pili kutokana na majeraha ya goti, lakini naamini uwezo wangu niliouonyesha mzunguko wa kwanza umewavutia Yanga na ndio maana wameamua kuniita na kutaka mazungumzo na mimi,” alisema.

Alisema anaamini iwapo atajiunga na mabingwa hao na kupewa nafasi na mwalimu ataweza kutimiza malengo yake kwa kuwa mfungaji bora kutokana na kikosi cha Yanga kujaa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU