DIAMOND PLATNUMZ AANIKA SIRI YA KUTOSWA BET

DIAMOND PLATNUMZ AANIKA SIRI YA KUTOSWA BET

1371
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA,

WAKATI msanii pekee kutoka Afrika Mashariki, Ray Vanny akitarajia kuhudhuria hafla za utoaji wa tuzo za BET, zinazotolewa Jumapili hii huko Los Angeles, Marekani, Diamond Platnumz amesema sababu za kutoswa kwenye tuzo hizo mwaka huu imetokana na kupunguza kasi ya kutoa kazi.

Akizungumza jana wakati akitambulisha nyimbo zake mbili mpya, I Miss You na Fire, Diamond alisema lengo lake la kupunguza kasi ya kutoa nyimbo lilikuwa ni kutoa nafasi kwa wasanii wengine.

“Mwaka jana sikutoa nyimbo, nilikuwa nifanya kazi ya kuwashika mkono wasanii pamoja na kuacha wenzangu nao wapate nafasi, ndiyo maana leo hii Ray Vanny anatuwakilisha vyema, lakini mwakani nitaingia tena kwenye tuzo hizo sababu nimeanza kuachia kazi,” alisema Diamond Platnumz.

Mwaka uliopita Diamond Platnumz aliingia kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa Afrika, ambapo alikutana na wasanii kam Black Coffee, Wizkid, AKA na Tiwa Savage.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU