WOLPER AOGOPA KUIBIWA ‘BABY’ WAKE NA MZUNGU WA HARMONIZE

WOLPER AOGOPA KUIBIWA ‘BABY’ WAKE NA MZUNGU WA HARMONIZE

1339
0
KUSHIRIKI

NA BRIGHITER MASAKI


MSANII wa filamu nchini, Jacqueline Wolper, amedai hataki tena kumweka wazi mpenzi wake mpya kwa kuogopa kuibiwa tena na wazungu.
Kijembe hicho cha staa huyo wa Bongo Movie, amekiachia kwenye mtandao wake wa Snapchat, kikihusishwa na tukio la mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, kuporwa na dada wa kizungu.
Papaso la Burudani lilizungumza na msanii huyo kuhusiana na kauli yake hiyo, lakini pamoja na kubanwa ili amtaje mpenzi wake huyo, alisema amefanya hivyo kufurahisha watu.
“Kuna wakati mwingine mtu anazungumza vitu ili kuwachekesha na kuwafurahisha watu, ila si kila unachozungumza ni kweli,” alisema msanii huyo huku akiangua kicheko.

mpenzi wake wa muda mrefu, Grace Mgonjo na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwamo wanasiasa na wasanii.
Baada ya ndoa yake kufungwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam, shughuli nzima ilihamia kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambapo kulifanyika tafrija iliyopambwa na watu maarufu mbalimbali.
Kwa upande wa wanasiasa, alikuwapo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na wengine wengi.
Kwa upande wa wasanii waliotumbuiza ni Diamond Platnumz, AY, Black Rhyno na Harmonize.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU