LUKAKU AMMWAGIA SIFA MOURINHO

LUKAKU AMMWAGIA SIFA MOURINHO

475
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

STRAIKA Romelu Lukaku amesema anavyoamini kocha wake, Jose Mourinho, ataweza kulipeleka soka lake katika hatua nyingine.

Mbelgiji huyo juzi alikamilisha vipimo vya afya  tayari kuwatumikia mashetani hao wekundu, baada ya kile kinachoaminika ada ya pauni milioni 75 ikubaliwe na Everton.

Lukaku alitumia muda wa misimu minne akiitumikia Toffees, baada ya Mourinho kumpiga bei wakati akiwa Chelsea kwa ada ya pauni milioni 28, baada ya kukipiga kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Goodison Park kwa muda wa mwaka mmoja.

Straika huyo alionekana kutofurahishwa na kuuzwa huko, lakini sasa anaonekana atakuwa tegemeo kwa Mourinho, kutokana na mmoja wa mastraika ambao wanahitajika Old Trafford, huku akiwa ameshakataa kurejea  Stamford Bridge kwa ajili ya kuungana na Mreno huyo.

“Mourinho ni mtu ambaye alinihitaji nicheze chini yake wakati nikiwa na umri wa miaka 10 na sasa nimepata nafasi tena ya kucheza chini yake, ni jambo la kujivunia,” staa huyo aliuambia mtandao wa ESPN.

“Tulikuwa tukiwasiliana akinieleza ni jinsi gani klabu inavyonihitaji na ni kitu gani anakitarajia kutoka kwangu,” aliongeza staa huyo.

“Unafahamu tulikuwa pamoja katika vipindi tofauti. Kwa ujumla tulikutana nikiwa bado ni kijana mdogo, nilikuwa na hamu ya kucheza. Na anafahamu uamuzi wangu wa kuondoka nilikuwa nahitaji kucheza,” aliongeza tena staa huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU