SZCZESNY ANUKIA JUVENTUS

SZCZESNY ANUKIA JUVENTUS

679
0
KUSHIRIKI

ROMA, Italia

MLINDA mlango wa Arsenal, Wojciech Szczesny, ananukia kukamilisha ndoto zake za kukipiga katika klabu ya Juventus, baada ya Gunners kumuacha katika ziara ya kujiandaa na msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Italia, Juve  wanamtaka mzuia mashuti huyo ili aweze kuwa mbadala wa nyota wao, Gianluigi Buffon, baada ya kufanya vizuri wakati akikipiga kwa mkopo katika klabu ya AS Roma.

Szczesny aliitumia misimu miwili iliyopita akiwa na klabu hiyo ya jijini Roma, kabla ya kurejea kikosini mwishoni mwa msimu uliopita, lakini ameendelea kusugua benchi nyuma ya Petr Cech, ambaye anaonekana kuaminiwa na kocha wake, Arsene Wenger.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU