…MASOGANGE AUGUA GHAFLA KISUTU

…MASOGANGE AUGUA GHAFLA KISUTU

870
0
KUSHIRIKI

NA KULWA MZEE,

MSANII Agnes Gerald Waya maarufu Masogange (28), ameumwa ghafla na kushindwa kusikiliza ushahidi dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili.

Kesi ya Masogange ilitakiwa kuanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa Jamhuri jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, alidai upande wa Jamhuri ulikuwa tayari kuendelea na kesi na shahidi yupo.

Wakili wa Masogange, Ruben Simwanza, aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu mteja wake ana tatizo la kiafya. Hakimu Mashauri alikubali kuahirisha kesi hiyo kwa sababu ushahidi hauwezi kuchukuliwa kwa sababu mshtakiwa anaumwa.

Kesi iliahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Masogange anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU