SIMBA KUFUATA DAWA YA YANGA A/KUSINI

SIMBA KUFUATA DAWA YA YANGA A/KUSINI

3084
0
KUSHIRIKI

NA SALMA MPELI,

PRESHA ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na mahasimu wao, Yanga utakaochezwa Agosti 23, mwaka huu imeanza kupanda.

Mchezo huo ambao utawakutanisha wafalme wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania, Simba, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika kuonyesha presha hiyo, Simba wamepanga kuondoka nchini Agosti 9, mwaka huu kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kusaka dawa ya kuifunga Yanga katika mchezo huo.

Kabla ya kwenda Afrika Kusini, Wekundu hao wa Msimbazi wataweka kambi mjini Morogoro kwa ajili ya kujiandaa na Tamasha la ‘Simba Day’ ambalo hufanyika kila mwaka Agosti 8.

Kocha wa klabu hiyo, Joseph Omog, alisema wataweka kambi Morogoro kwa muda mfupi kujiandaa na mechi yao ya Simba Day na kuondoka nchini.

“Tutakuwa na kambi ya wiki moja mjini Morogoro kabla ya kuondoka kwenda Afrika Kusini,” alisema kocha huyo.

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilianza mazoezi tangu wiki iliyopita katika Uwanja wa Chuo cha Polisi uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU