AZAM MMEMFANYA NINI MIGI?

AZAM MMEMFANYA NINI MIGI?

3028
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

KIUNGO wa zamani wa Azam FC ambaye sasa anakipiga Gor Mahia ya Kenya, Jean-Baptiste Mugiraneza `Migi`, amesema hana fikra za kurejea kucheza soka Tanzania.

Migi ambaye ni raia Rwanda, aliwahi kukipiga Azam FC kabla ya timu hiyo kuamua kusitisha mkataba wake.

Kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Gor Mahia kilichocheza dhidi ya Everton ya England katikati ya wiki katika pambano la kirafiki na timu yake kuchapwa mabao 2-1.

Migi ameliambia BINGWA kuwa hayupo tayari kurejea kucheza soka katika ardhi ya Tanzania, kwa madai kwamba uongozi wa Azam ulimfanyia kitu kibaya wakati akiitumikia timu yao.

“Mimi kwa sasa ni mchezaji Gor Mahia lakini pia nahitaji kusonga mbele zaidi na si kurudi nyuma ndio sifikirii kurejea tena kucheza soka Tanzania,” alisema.

Migi alisema anaimani Gor Mahia ni njia sahihi kwake ya kumfanya atimize ndoto zake kutokana na namna nzuri ya uendeshaji wa klabu hiyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU