MKWASA AMSHANGAA MWAMBUSI KUFUNGASHA ‘KIENYEJI’

MKWASA AMSHANGAA MWAMBUSI KUFUNGASHA ‘KIENYEJI’

3626
0
KUSHIRIKI

NA MAREGES NYAMAKA

KATIBU Mkuu wa Yanga, Charles  Mkwasa, ameshangazwa na hatua ya aliyekuwa kocha msaidizi wa  timu hiyo, Juma Mwambusi, kutangaza kuondoka Jangwani.

Kocha huyo hivi karibuni alitangaza kujiweka kando na shughuli za soka kwa muda, baada ya mkataba wake na waliokuwa waajiri wake klabu ya Yanga kumalizika.

Akizungumza na BINGWA, Mkwasa alisema taarifa za Mwambusi  kutoendelea kuifundisha timu hiyo amezisikia kupitia vyombo vya habari, hatua aliyodai imemshangaza kwakua kocha huyo hakuwahi kumfuata ofisini kwake na kuzungumza naye kuhusiana na mustakabali wa ajira yake.

“Nimesikia tu kwenye vyombo vya habari lakini hatujakaa tukaongea hilo suala, lakini kama kaamua hivyo sawa hamna namna, klabu ina utaratibu wake kama kutakuwa na mabadiliko tutawajulisha,” alisema Mwambusi.

Mwambusi hajaonekana katika mazoezi ya Yanga yaliyoanza rasmi siku ya Jumanne wiki hii, huku kukiwa na taarifa kuwa beki wa zamani wa timu hiyo, Shadrak Nsajigwa, amechukua nafasi yake.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU