NDUDA: SIMBA LETENI SH MILIONI 60 NISAINI

NDUDA: SIMBA LETENI SH MILIONI 60 NISAINI

3169
0
KUSHIRIKI

NA CLARA ALPHONCE

KIPA bora wa michuano ya Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), Said Mohamed ‘Nduda’, amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itakuwa tayari kumpa kitita cha Sh milioni 60.

Nduda kwa sasa yuko huru baada ya mkataba wake na klabu aliyokuwa akiitumikia ya Mtibwa Sugar kumalizika msimu uliopita.

“Mimi dau langu ni Sh milioni 60, timu itakayonipa hizo fedha niko tayari kuichezea,” alisema Nduda.

Kuhusu uwezekano wa kujiunga na Simba ambayo imehusishwa kumwania alisema;

“Tupo kwenye mazungumzo kama watakuwa tayari kutekeleza masharti yangu nitasaini, ila kwa sasa sijaridhika na dau lao,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU