DIVA AJIPITISHA KWA KIBA, ‘MOND’

DIVA AJIPITISHA KWA KIBA, ‘MOND’

1230
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA


MWIMBAJI anayezidi kuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’, ameanza kufuata nyayo za wakali wa muziki huo, Ally Kiba na Abdul Nassib ‘Diamond’, kwa kujitangaza kimataifa kwa kufanya ‘tour’ yake ya kwanza nchini Kenya, iliyomkutanisha na wadau mbalimbali.

Akizungumza na Papaso la Burudani kutoka Nairobi, nchini Kenya, msanii huyo alisema ziara hiyo itamsaidia kupata mashabiki wapya na kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania.

“Ili kujitangaza kimuziki lazima kuwafuata mashabiki wako walipo, sasa nipo Kenya huku katika ziara yangu. Pia nimepanga nizunguke Afrika Mashariki nzima kujitambulisha zaidi,” alisema Lulu Diva.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU